DMI INA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI WA BLUU, YAWAKARIBISHA WANAFUNZI KUJIUNGA

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI),kimesema kuwa elimu inayotolewa na chuo hicho inahusiana na uchumi wa bluu ambapo kwa sasa serikali inasisitiza kuwekeza katika uchumi huo.

DMI ni chuo cha serikali kipo chini ya Wizara ya Uchukuzi ambacho kina majukumu matatu kutoa elimu na mafunzo kwa upande wa bahari, kutoa ushauri elekezi kwa taasisi za Umma na serikali pamoja na kufanya tafiti zinazohusiana na sekta ya bahari.

Akizungumza leo Agosti 04 katika maonesho ya wakulima na Wafugaji ( Nane nane ), ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma kwenye banda la chuo hicho, Msimamizi kitengo cha usajili wa wanafunzi kutoka DMI Bernard Mgendwa amesema kuwa wanauhusiano mkubwa na maonesho hayo kwa kuwa wanatoa masomo yanayolenga uchumi wa bluu.

Mgendwa ameeleza kuwa wanatoa elimu sahihi ya vifaa vya uokozi, namna ya kujiokoa wanapopata shida kwenye maeneo ya bahari na ya maziwa makuu. 

" Tupo katika maonesho haya, tunatoa huduma ya kusajili wanafanzi wanaomba kwa ajili ya kujiunga na chuo hiki , pia tunatoa ushauri kwa kozi za kusoma wanafunzi waliofauli na kuwaelekeza ufaulu ambo unaweza kumfanya mwanafunzi kujiunga na chuo hiki," amesema.

Msimamizi huyo ameongeza kuwa katika upande wa mafunzo wana sehemu mbili waliosoma masomo ya Art na Sayansi ambapo wanatoa elimu kuanzia ngazi ya cheti hadi masters.

"Kwa wale waliosoma ngazi ya shahada kwa upande wa Sayansi tunatoa elimu ya Uhandisi na unahodha na oparesheni kwa upande wa bandari hii ni kwa waliosoma masomo ya art," ameeleza.

Amefafanua kuwa ili mwanafunzi aweze kujiunga na masoma hayo lazima awe na alama D 2 kwa masomo ambayo sio ya dini na kwa wanaotaka kujiunga ngazi ya cheti wawe na alama D 4.

Msimamizi huyo amesema usajili unaendelea hadi Agosti 10, mwaka huu na kwamba kutakuwepo na awamu ya pili ambayo itaanza Septemba 3, nakufungwa Septemba 21 na ngazi ya cheti awamu ya pili usajili unaanza Agosti 5, mwak huu.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI