VETA YAJIPANGA KUHAKIKISHA WAKULIMA NCHINI WANALIMA KILIMO CHENYE TIJA

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore amesema mamlaka hiyo imejipanga katika kuhakikisha Wakulima nchini wanalima Kilimo chenye tija kutokana na teknolojia mbalimbali zilizobuniwa na vyuo vya VETA.

Pia amesema katika maonesho ya wakulima na Wafugaji (Nane nane), wamekuja na mashine ya kutengeneza udongo kwa ajili ya kuoteshea mazao ya bustani ambapo udongo wa kuoteshea ulikuwa umatoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ukilinganisha na mashine iliyopo VETA ni ya gharama nafuu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 04,2024 katika banda la VETA kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma amesema kuwa VETA katika Maonesho imekuja na teknolojia ambazo zitafanya Kilimo nchini kukua kutokana kwa kupata mashine za gharama nafuu kupatikana.

CPA Kasore amesema vyuo vya 80 vimeshajengwa katika Mikoa na Wilaya huku vyuo 65 vipya vinajengwa katika Wilaya na kufanya kila Wilaya kuwa na Chuo cha Ufundi Stadi.

Aidha amesema kuwa vijana na wananchi watumie vyuo hivyo wananchi na vijana kutumia fursa katika kupata ujuzi na kuweza kujiajiri.

Ameongeza kuwa VETA imegusa fani katika kila Chuo kuendana na mazingira yake lengo ikiwa ni kufanya mhitimu kutafuta soko lake bila kukabiliwa na changamoto.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI