TSB KUONGEZA VITUO VYA USINDIKAJI ZAO LA MKONGE NCHINI

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB), kwa kusrikiana na Wizara ya Kilimo imeweka mpango wa kuweka vituo vya usindikaji wa zao la mkonge lengo likiwa ni kumsaidia mkulima mdogo ili aweze kusindika na kupata nyuzi, singa ambazo zitakubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma katika maonesho ya wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa viwanja vya nane nane Nzuguni jijini hapa na 

Mkuu sehemu ya Maendeleo ya Mkonge kutoka TSB Saimon Kibasa amesema Bodi imekuwa ikiwaunganisha wakulima na masoko na kwamba  sehemu ya  masoko hayo ni  kuwaunganisha  wakulima hao ili wapate soko la bei nzuri.

Ameongeza kuwa nchini Tanzania wakulima wamegawanyika katika makundi matatu wadogo, wakubwa na wakati  huku akisema  wakulima wakubwa hawana changamoto kama ilivyo kwa wakulima hao wadogo.

"Na wakulima wadogo nao wamegawanyika katika sehemu mbili wanaolima kwenye mashamba yao binafisi na wanaofanyabiashara  lakini wapo ambao wanalima  kilimo cha mkataba kinachoendeshwa katika mashamba matano nchini yakiwamo Ngombezi na magoma," amesema.

Amefafanua kuwa katika mashamba hayo yana mikataba kati ya mkulima mdogo na Bodi ambapo inamkodisha mkulima huyo na kazi yake ni kulima na kutunza mkong na kwamba kuna mkataba kati ya vyama vya ushirika vilivyopo katika mashamba hayo na usindikaji.

"Wote hawa wanasimamiwa na Bodi kwa kushirikiana na ofisi ya Msajili wa vyama vya ushirika Mkoa wa Tanga katika maeneo hayo TSB imekuwa ikiwasimamia wakulima kuhakikisha wanapata bei nzuri kupitia wanunuzi mbalimbali.

Kibasa ameongeza kuwa lengo la kuhamasisha kilimo hicho ni zao ambalo lina soko kubwa na ni zao ambalo linastamili magonjwa, ukame na ni la uhakika kumpatia mkulima kipato.

Bodi hiyo ni Taasisi ya serikali ambayo ipo chini wizara ya kilimo ni msimamizi na mhamasishaji maendeleo ya mkonge nchini.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI