PURA: MKULIMA KWETU NI MDAU MUHIMU, YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

Na Mwandishi wetu, Dodoma 

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa wakulima wakati wa utekelezaji wa miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia inayotekelezwa nchini imeshiriki maonesho ya Nane Nane mwaka huu kueleza nafasi ya wakulima katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Hayo yamesemwa leo Agosti 03,2024 jijini hapa katika maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya nane nane Nzuguni na Mjiolojia kutoka PURA Ebeneza Mollel amesema kuwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia sekta ya kilimo na sekta ya mafuta na gesi asilia zinategemeana.

Mollel ameeleza kuwa miradi hiyo inahuaisha mkusanyiko wa idadi kubwa ya watu, ikiwemo wafanyakazi na vibarua katika maeneo inakotekelezwa miradi hiyo, ambao hutegemea chakula kinachotokana na mkulima. 

"Bila kuwapo kwa mkulima ni dhahiri kuwa utekelezaji wa miradi itaathirika. Hivyo, kwetu sisi, mkulima ni mdau muhimu na ndio maana tunashiriki maonesho haya" alieleza Mollel .

Mollel amesema mbali na wakulima kuwa chanzo cha chakula kwa watu wanaofanya kazi katika miradi ya mafuta na gesi asilia, gesi hiyo inayozalishwa nchini inaweza kutumika kuzalisha mbolea hivyo kuwanufaisha wakulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.

"Ingawa kiwanda cha kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia bado hakijajengwa nchini, Serikali kupitia mamlaka zake imeendelea kuweka juhudi kuhakikisha viwanda hivyo vinajengwa" aliendelea Mollel.

Ameongeza kuwa katika maonesho hayo PURA imetumia fursa ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji kuhusu Shirika hilo linavyoshirikiana na wadau wake.

Hata hivyo Mollel amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la PURA ili kujifunza mambo masuala ya Uzalishaji wa mafuta na gesi asilia inavyopatikana.

PURA, kama mdhibiti na mshauri wa masuala ya mkondo wa juu wa petroli, ina jukumu la kuhakikisha, pamoja na mambo mengine, uhakika wa upatikanaji gesi asilia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mbolea

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI