TAEC: MIONZI INATUMIKA KUHIFADHI CHAKULA, YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NANE NANE DODOMA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MTAALAM wa Mionzi kutoka Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Alphonce Mgina amesema kuwa mionzi kwenye kilimo inatumika kuhifadhi chakula ili kiweze kukaa kwa muda mrefu.

Hayo ameyasema leo Agosti 03, 2024 jijini hapa katika maonesho ya wakulima na wafugaji (nane nane),yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma Mgina amesema kuwa kupitia mionzi wameweza kuua baadhi ya wadudu ambao ni wasumbufu kwenye mazingira.

"Kwenye maonesho haya TAEC imekuja kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuweza kupambana na mionzi kwa kuwa inafaida katika maisha ya binadamu na pia ikitumiwa visivyo huwa inapeleta madhara," amesema.

Ameeleza kuwa Taasisi hiyo inajipambanua kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ili waweze kupata huduma za mionzi hiyo huku akisema kama wanaenda hospitali waweze kupata huduma za mionzi inayofaa.

Mgina ameongeza kuwa Tume hiyo inaangalia mionzi kupitia vyakula ubora na uchafuzi hivyo TEAC imeweka vituo katika viwanja vya ndege bandari na mipaka kwa ajili ya kukagua vyakula vinavyoingia kama vimechafuliwa na mionzi.

Ameeleza kuwa TEAC inaangalia vyakula vinavyosafirishwa kutoka nchini kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kulinda soko la Tanzania.

"TEAC imeweka watumishi wengi kwa lengo la kupambana na hili endapo kuna tatizo la mionzi Tume inakuwa ya kwanza kupambana na tatizo hili," ameeleza.

Akizungumzia maonesho hayo ya nane nane ameeleza kuwa mwitikio wa watu kutembelea banda la TAEC ni mkubwa kwa kuwa wanatamani kujifunza mionzi ni nini huku akisema wengine ni wasafirishaji wa vyakula

Aidha amewataka watembeleaji wa maonesho hayo kutembelea banda la TAEC ili waweze kujionea faida za mionzi na hasara pale itakapotumika vibaya.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI