RITA YAHUDUMIA WATU ZAIDI YA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

TIMU ya wataalam wa kutosha kutoka makao makuu Dodoma na Dar es Salaam wameungana kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi wanaotembelea banda la Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), ambapo zaidi ya watu 500 wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Wakala huo pia unatoa huduma za usajili na vyeti vya vifo, usajili wa bodi za wadhamini, usajili wa ndoa na talaka, kuandika na kuhifadhi wosia, usimamizi wa mirathi na msaada wa kisheria bila malipo. 

Akizungumza leo Agosti 8,2024 na Waandishi wa habari katika banda la wakala huo kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayoendelea kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Afisa Mawasiliano wa RITA, Jafari Malema, ameleza kuwa watu wengi wamejitokeza kufuatilia vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya vifo pamoja na vya ndoa katika maonesho hayo.

Malema amesema walianza kutoa huduma mbalimbali za usajili na vyeti vya kuzaliwa tangu Agosti Mosi na kwamba wataendelea kuwepo katika maonesho hayo hadi Agosti 10 mwaka huu.

" Tumewarahisishia wananchi huduma ya kusajili vyeti vya kuzaliwa na vifo tumeiweka kidijitali anaweza akajisajili popote alipo alipo kwa kutumia mfumo wetu wa E – Rita na akija na fomu aliyoipakua kutoka kwenye maombi yake tunampatia cheti chake ndani ya saa 24. 

Ameongeza kuwa huduma hiyo ya kidigitali imewapunguzia wananchi gharama pamoja na muda wake ambao atautumia katika kufanya shughuli zake za kiuchumi.

Akizungumzia wa usajili wa wosia amesema kuwa bado kuna changamoto kidogo huku akisema wananchi wamekuwa na woga ambapo anahisi akiandika wosia huo anakaribia kufariki,kupoteza maisha.

"Tunaendelea kutoa elimu watu wafahamu umuhimu wa kuandika wosia kwa kuwa baadhi ya watu wana mtazamo kwamba ukiandika wosia unajichulia wakati si kweli" ameeleza.

Ameongeza kuwa lengo la wosia huo ni kuepuka masuala ya migogoro inayosababishwa na Wana familia kugogombania Mali mara baada ya muhusika kufariki.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI