UDOM YAWAHAMASISHA WAKULIMA , WAFUGAJI KUTUMIA MBINU NA TEKNOLOJIA KWENYE KILIMO, YAWAKARIBISHA WANAFUNZI KUFANYA UDAHILI

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimewahamasisha wakulima kutumia mbinu na teknolojia mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi walizozibuni kwa lengo la kuongeza tija na kukuza sekta ya kilimo.

Akizungumza leo Agosti 3, 2024 kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko UDOM, Rose Mdami, amesema  miongoni mwa teknolojia zinazooneshwa na chuo hicho katika maonesho hayo ni kifaaa cha kulishia samaki kinachotoa tarifa kwa mfugaji kuhusu muda na kiasi cha chakula.

Amesema kuwa wanataaluma wa chuo hicho kwa kushirikiana na wanafunzi wamekuwa wakifanya tafiti na kubuni teknolojia mbalimbali ambazo ndio njia pekee ya kuwainua wakulima.


Mkuu huyo wa kitengo ameeleza kuwa kwenye maonesho  hayo chuo hicho kimekuja na bidhaa zinazohusiana na kilimo  lengo lao  ni kushiriki kwa kutumia wanataaluma wake katika  suala zima la kuendeleza na kukuza kilimo.


Ameongeza kuwa chuo cha UDOM kinafundisha sayansi na kinazalisha wanataaluma na wanasayansi na teknolojia zinazotumika katika uzalishaji mkubwa wa kilimo,” amesema Mdami

Amesema wanahakikisha chuo kinakuwa na mchango katika kuhakikisha mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia yanayotokea duniani yanatumika kuendeleza na kukuza sekta ya kilimo.

Amesema bidhaa nyingi za kilimo wanazoonesha kwenye maonesho hayo zimetokana na tafiti ambazo chuo kinaendelea kufanya na kutolea mfano Mkoa wa Dodoma ambao hauna mvua nyingi kwa kubuni mazao ambayo yanastahimili ukame.

“Tunaamini tukiendelea kufanya hivyo tutazalisha wataalam ambao watakwenda kusaidia jamii ikajifunza kutoka chuo kikuu cha Dodoma tukaendelea kuongeza uzalishaji na wananchi kupenda na kujihusisha na kilimo," amesema.

Katika hatua nyingine amesema kuwa kwenye maonesho hayo chuo hicho kinafanya udahili kwa wahitimu wa kidato cha sita na wale waliomaliza diploma na kuwataka wanaotaka kujiunga kuanzia ngazi ya stashahada, shahada za awali na shashada ya uzamivu kutembelea katika banda la Udom.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI