VETA TABORA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUPATA MAFUNZO YA USEKETAJI

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Tabora imewakaribisha Watanzania kwenda chuoni hapo kupata mafunzo ya Useketaji ambayo yanatolewa na chuo hicho pekee.

Pia Mamlaka hiyo imetoa wito kwa serikali kufufua viwanda vya nguo ili iwe rahisi kuwaajiri vijana wa kitanzania kuweza kuzalisha Viwanda vyetu vya nguo ambapo viwanda vingi vya nguo vilibinafsisha na waliopewa wameshindwa kuviendeleza.

Hayo yamesemwa leo Agosti 3, 2024 katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma na Mwalimu wa Useketaji kutoka VETA Tabora, Diana John wanapokea wanafunzi wa aina mbalimbali.

Amesema wana mashine za aina mbili, mashine ya mezani na mashine ya kuweka chin na kwamba Mashine ya mezani ni kwa mtu yeyote hata kama ni mzee anachukua mashine yake anaiweka mezani, na kuanza kutengeneza vitambaa vidogo vidogo. 

Mwalimu huyo amesema ujuzi huo wa Useketaji unapatikani Veta Tabora pekee ambapo wanatengeneza vitambaa vya aina mbalimbali, vikoi, mashuka, mabedi cover pamoja table max.

Amefafanua mashine hiina uwezo wa kutengeneza vitu vya aina mbalimbali, ambapo wanatengeneza kwa kutumia nyuzi ambazo zimetengenezwa kwa pamba za hapa hapa Tanzania.

 "Karibuni VETA Tabora, leteni watoto ili waweze kupata ujuzi wa useketaji mtoto atakapo maliza anakuwa ameshapata ujuzi wa ambapo atajiari mwenyewe badala ya kusubiri ajira serikalini ameeleza.

Amefafanua kuwa muitikio wa wanafunzi kwenye kozi hiyo sio mkubwa kutokana na ajira zake hazipatikani kwa wingi.

Mwalimu huyo ameongeza kuwa kipato cha Mtanzania sio kikubwa kutokana na mashine hii moja mtu anaipata kwa Shilingi milioni 1.5 na mashine ndogo ni 150,000 ambayo ni kwa uzalishaji mdogo, mtu akitaka uzalishaji mkubwa lazima anunue mashine hii kubwa, " amesema.

Hata hivyo ameiomba serikali ivirudishe viwanda hivi ili kusaidia katika kuongeza ajira katika eneo hili. 

Pia wazazi walenge watoto kujitegemea na wasifikie kuajiriwa kwasababu hiyo fani kwa mzazi mwenye malengo anaweza kumleta kijana wake au yeye mweyewe akasoma kozi fupi ambapo atengeneza pesa nyingi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI