WALIOTEMBELEA BANDA LA GCLA WAMETAKA KUJUA MASUALA YA KEMIKALI NA VINASABA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),imesema kuwa idadi kubwa ya maswali yaliyoulizwa na wananchi waliotembelea banda la mamalaka hiyo katika maonesho ya wakulima na Wafugaji (Nane nane), yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma wametaka kufahamu kuhusu masuala ya kemikali na vinasaba vinavyofanya kazi.

Akizungumza leo Agosti 7,2024 katka maonesho hayo kwenye banda la Mkemia Mkuu wa Serikali Meneja Kanda ya Kati kutoka mamalaka hiyo Gerald Mollelamesema kuwa wengi waliotembelea banda la Mamlaka hiyo maswali yao makubwa yanahusu kemikali na vinasaba.

Meneja huyo ameeleza kuwa watembeleaji hao wamewataka kujua vinasaba vikoje na ni namna gani ya kupima mtoto.

"Majukumu yetu mengi yanahusisha uchunguzi wa sampuli ambazo zinahusiana na makoasa ya jinai, sampuli za chakula, mazingira, zinazohusiana na dawa za asili na za kisasa zinazohusiana kushtukia na zinazohusiana na vinasaba za binadamu," amesema.

Akizungumzia maonesho hayo amesema Mamlaka hiyo inauhusiano mkubwa na wakulima Wafugaji ambapo inafanya uchunguzi mbalimbali wa vyakula huku akiwakaribisha Wakulima hao kutembelea banda la Mkemia Mkuu wa Serikali ili waweze kupata elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na GCLA.

Amesema kuwa kwa wananchi ambao wapo vijijini wanawafikia kwa njia ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na semina mbalimbali.

Ameongeza kuwa GCLA inafanya uchunguzi wa sampuli nyingi ambazo ni za jinai zikiwamo za mauaji ambapo Mkemia Mkuu anapochinguza na kutoa ushahidi mahakamani.

Naye Kaimu Mkurugenzi Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka GCLA,Dk. Shimu Peter amesema kuwa katika shughuli zao zote za uchunguzi Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa Sheria Namba 9 ya mwaka 2016 ni Mamlaka ya rufaa nchini katika shughuli hizo za sampuli na vielelezo mbalimbali.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa majukumu yao mengine ni kusimamia Sheria ambapo wana Sheria hizo kuu tatu.

Amezitaja Sheria hizo kuwa ni ya vinasaba vya binadamu ya mwaka 2009 na Sheria nyingine ya kudhibiti kemikali za viwandani na majumbani, Sheria Namba 3 ya mwaka 2003 na ya mamalaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambayo ni ya mwaka 2016, Mamlaka imepewa jukumu hilo la kuhakikisha utekekezaji wa Sheria hizo unakidhi viwango, zinatekelezeka.

Akitole mfano Sheria ya kwanza ya vinasaba ambapo amesema watu wote wanahusika wanataka kufanya shughuli za Tume ya teknolojia ya vinasaba hivyo wawe wamesajiliwa na Mamlaka ya GCLA.

Dk. Peter ameeleza kuwa kwa wale wanaohusika na kemikali Sheria Namba 3 ya mwaka 2003 inawahusu na inawataka wawe wamesajiliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye Msajili wake na waingizaji wa kemikali hizo, wasafirishaji, watumiaji na watunzaji kwa mujibu wa sheria wanatakiwa wawe wamesajiliwa.

Amefafanua kuwa Sheria ya tatu ambayo ni GCLA inawataka watu wote ambao wana maabara lazima wawe wamesajiliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali.

Dk. Peter ameongeza kuwa katika jukumu lake jingine la Mamlaka hiyo ina kituo cha kuratibu matukio ya sumu ambapo watu wote wanashughulika na madhara yote ya sumu GCLA ina kituo cha kanzidata ya sumu zote nchi ambapo imekuwa ikifanya shughuli zote za kuwasiliana na watoa huduma wa afya ili kuweza kunusuru maisha ya watu ambao bado hawajafariki, wamedhurika ili matibabu sahihi yaweze kutolewa kulingana na dawa sahihi ambayo zimemuathiri

Aidha amewakaribisha wananchi kutembelea banda hilo ili waweze kupata elimu mbalimbali zinazohusiana na shughuli ambazo zinafanywa na mamalaka hiyo ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI