Dar es Salaam
KAMATI ya Siasa, Sekretarieti ya Kata pamoja na WDC ya Kata ya Saranga imeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutekeleza na kushusha miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutatua kero za wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Serikali iliyotekelezwa katika Kata ya Saranga, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Saranga, Ndugu Salum Nasoro Kibanda, ameipongeza Serikali kwa juhudi za kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi.
Ziara hiyo iliyoandaliwa na Mheshimiwa John Sanga, Diwani wa Kata ya Saranga, ilikuwa na lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuanzia Novemba 2025 hadi Julai 2026.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kituo cha Afya/Zahanati ya Saranga, Daraja la Magongo, Temboni Water Boosting, pamoja na miradi mingine iliyotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu na Mfuko wa Jimbo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa John Sanga alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya Kata ya CCM kwa kuendelea kuisimamia Serikali na kuhakikisha ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni zinatekelezwa kwa vitendo.
Viongozi hao wameeleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii na miundombinu, pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Kata ya Saranga.
Imetolewa na:
Ofisi ya Diwani, Kata ya Saranga



0 Comments