Chifu Mkuu kanda ya kati Henry Mtemi Mazengo II, wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WAKATI mwingine wanajamii hutumia haki za kitamaduni kama kisingizio cha kukandamiza wengine ,kubinya haki zingine za binadamu katika jamii jambo ambalo sio kweli.
Haya yamesemwa leo Februari 10,2022, jijini Dodoma na Chifu Mkuu kanda ya kati Henry Mtemi Mazengo II, wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku chache kupita tangu Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole kutoa kauli tata ya kuubeza utawala wa kichifu na kusema kuwa mchifu hawana lolote na kuomba utamaduni uheshimiwe.
Amesema watanzania wanapaswa kuheshimu mila na desturi za kitanzania kwa kuwa zina mchango mkubwa katika jamii na endapo zitaenziwa zitasaidia kuwepo kwa heshima ya haki za binadamu .
Chifu Mazengo zamani walikuwa na utawala wa machifu, masultani na wafalme ili kuhakikisha watawala wanafanya kazi zao sawasawa na kwa kwamba himaya zilikuwa na vyombo vyake.
Amefafanua kuwa kulikuwa himaya za majeshi,usalama, elimu, sanaa vyote hivyo vilihakikisha masilahi ya uchumi na usalama wa raia na kwamba utaratibu ni huo huo.
Chifu Mazengo amesema suala la Mbunge huyo wa kuteuliwa la kusema utawala wa Machifu si lolote si chochote linaleta ukabila na mgawanyo Katika jamii wakati halina mashiko hivyo kutaka kila mtu kwa nafasi yake kulikemea.
"Taarifa hizi zinaligawa taifa na likichukuliwa kimzaha mzaha litarudisha chuki za ukabila,si SW la kulikalia kimya hata kidogo lazima tulikemee,"anasisitiza
Mbali na hayo ameeleza kuwa utawala wa kichifu hauna nia mbaya kwa taifa bali kuhakikisha jamii inakaa kwenye mstari na kuisaidia jamii kuepuka kwenda kinyume na utaratibu wa Mila na desturi.
"Polepole anapaswa kufahamu kuwa machifu tuna umoja wetu ambao unaisaidia Serikali kuhifadhi Mila zetu Kwa vizazi vijavyo na ndio maana serikali inatambua na kuthamini mchango wetu,"amesema.
Aidha,Chifu Mazengo amesema ni muhimu kwa watanzania wote kuungana kwa pamoja kulinda amani ya Tanzania si kukaa na kushabikia kauli zinazoleta mkanganyiko katika jamii.
Hata hivyo Chifu Mazengo ameshauri viongozi wote kuwa mstari wa mbele kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhi Hassan kukemea vitendo viovu mara vinapotokea bila kusubiri Rais aongee.
Aidha amesema kuwa kabla ya wakoloni, walikuwa na namna zao za kuendesha mambo huku akidai kwamba kwa sasa mambo yamebadilika.
"Machifu tunabaki kwenye nafasi yetu lakini kuna Viongozi wengine wanapaswa kusimama na kukemea haya maovu ya kudharau masula ya mila na desturi"amesisitiza Chifu hiyo.
0 Comments