Naibu Waziri wa Afya akifanya usafi katika soko la Mavunde lililopo Chang'ombe Kata ya jijini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga akisafisha mtaro ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ilianza Jumatatu Februari 7 mwaka huu kwa kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wadau.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
GHARAMA ya kusafisha mazingira ni ndogo kuliko ya kwenda hospitalini kutibu magonjwa yatokanayo na mazingira ambayo ni machafu katika maeneo yanayoizunguka jamii.
Pia amewataka wakazi wa Dodoma kufanya usafi ili kupunguza gharama zitokanazo na kununua dawa ili kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu na badala yake zitawasaidia kwa matumizi mingine.
Hayo yamesemwa leo Februari 10,2022, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dk.Goodwin Mollel wakati wa zoezi la kuelimisha wafanyabiashara wa Soko la Mavunde lililopo Chang'ombe Kata ya Chang'ombe,kuhusu kutenganisha taka ngumu na zinaooza ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,amesema kuwa watu wengi wanaugua na kupoteza maisha kwa sababu ya uchafu wa mazingira.
Dk.Mollel ameongeza kuwa mtu anapo ugua mgonjwa ambayo yatokanayo na uchafu wa mazingira akienda hospitali kutibiwa atatumia gharama si chini ya 600,000 hivyo ni vema kuyatunza.
"Lakini pia unaweza kufanya biashara yako na faida yako ukaitumia kwa matumizi mengine ikiwa unafanya mazingira," ameongeza na kusema kuwa.
"Nawashukuru sana watendaji ambao mnafanya kazi hii mnaweza kusafisha na kutunza mazingira lakini kumbe mnatupunguzia bajeti ya dawa hospitalini," amesema Dk.Mollel.
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kila mmoja ahakikishe anampatia mti mtoto wake kwenda kupanda na kutunza shuleni.
Magonjwa ya mlipuko yanatokana na uharibifu wa mazingira kama vile kukata miti hivyo na kutolea mfano wadudu kama nyoka wanatoka porini kufuata makazi ya watu kutokana na uharibifu huo.
"Mwezi huu Februari kulikuwa na wagonjwa watu ambao hawajachanja lakini waliochanja walipata homa kidogo na wakaendelea na shughuli zao," amesema.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga amesema wiki hiyo ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ilianza Jumatatu kwa kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi na wanafunzi.
Aidha amesema wananchi wa kata ya Chan'gombe wamefundishwa jinsi ya kutenganisha taka ngumu na taka zinaweza kuoza ili kuzuia mrundikano wa taka ngumu.
Naye Afisa Mazingira jiji la Dodoma Ally Mfinanga amewataka wananchi kupeleka taka zinazooza jalalani (Dampo), kwani wanampango wa muda mrefu kukutengeneza gesi kutokana na taka hizo zinazooza.
Amesema kuwa ushindiliaji wa taka Dampo hautafanyika vizuri kama kila aina ya taka zitapelekwa huko na kwamba kuna aina ya taka za karatasi ambazo zinaweza kutumika zaidi mara mbili.
Amesema kuwa wao kama Halimashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, wameamua kutatafuta vifaa vya kutenganishia taka lengo likiwa ni kupunguza kiwango cha taka kinachoenda kutupwa jalalani (Dampo).
Ameongeza kuwa taka za plastiki ni mali, mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu na wafanyabiashara wakakusanya taka hizo na kwenda kuuza ambapo wanajipatia kipato.
" Leo tupo hapa sokoni lengo letu ni moja kuwafundisha wafanyabiashara ni nmna gani tunaweza kutenganishia taka zinazooza na zile za plastiki," amesema.
Ameeleza kuwa wafanyabiashara hao wanaweza kutumia taka za kuoza kama mabaki ya chakula Cha kuku,kutengeneza chakula cha mifugo na mbolea kutokana nantaka hizo.
Wakazi, wafanyabiashara na wakazi wote wa Dodoma wajifunze kutenganishia taka hiyo inasaidia hata kwenye vyombo vya usafirishaji hadi Dampo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Mavunde lililopo Chang'ombe Kata ya Chang'ombe Gofrey Mbilinyi amesema kuwa kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake usafi huo wameupokea na wanauunga mkono pamoja na elimu ya utunzaji mazingira waliipata.
0 Comments