Mboga mboga
Na Asha Mwakyonde
ULAJI bora ni ule unaozingatia ushauri wa wataalamu kwani kumekuwa na tabia ya watu kula vyakula bila kuzingatia mahitaji ya miili yao.
Wataalamu wanashauri kula vyakula kulingana na rika husika lakini pia kufanya mazoezi ili kujenga mwili na kuuweka sawa.
Tunapokula zaidi na hatufanyi mazoezi ya kujenga mwili, tunaweza kupata uzito au unene mwingi kupita kiasi.
Ofisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Abela Twin'omujuni anazungumzia ulaji unaofaa kwa kundi la vijana
balee anasema kulingana na tafsiri ya Shirika la Afya Duniani (WHO),kuna vijana balee wa kundi la kwanza ambao ni kuanzia umri wa miaka 10
hadi 19.
Ofisa huyo anafafanua kuwa kundi la vijana balee umri wa kwanza ni miaka 10 hadi 15 na umri wa mwisho ni miaka 15 hadi 19.
Twin'omujuni anaeleza kuwa lishe ni muhimu kwa kundi la vijana balee kwa sababu ni umri ambao ni kipindi cha pili cha ukuaji wa haraka
kinaotokea katika kundi hilo.
Anasema kipindi cha kwanza ni tangu mtoto akiwa tumboni hadi kufikia umri wa miaka miwili.
"Kutokana na ukuaji wa haraka unaotokea katika kundi hili wanahitaji chakula cha kutosha kutoka katika makundi matano ya chakula ili
kukidhi mahitaji muhimu ya miili yao ikiwamo, ukuaji wa kiali, kisaikolojia na kimwili, "anasema.
Anaongeza kuwa umuhimu wa lishe kwa vijana hao ni kukabili mahitaji mengine yanayowakabili mfano wanahitaji kupata viturubishi vya
vitamini na madini ambayo ni muhimu katika ukuaji wao.
Twin'omujuni anasema virutubishi hivyo vinapatikana kwenye vyakula
kutoka kundi la mboga mboga na matunda ambavyo vipo katika makundi
matano ya chakula.
Anafafanua kuwa kundi la kwanza ni nafaka, mizizi na ndizi ambalo linatoa kirutubishi kwa ajili ya kutia mwili nguvu.
Mtafiti huyo anabainisha kuwa kundi la pili ni la vyakula vya asili ya wanyama na jamii ya kunde kunde ambavyo hupatia mwili mafuta na kundi
la tatu ni mboga mboga za majani na zisizo za majani kama vile karoti na nyanya, kundi la nne ni matunda.
"Kundi hili la mboga mboga na matunda linasaidia katika kuupatia mwili vitamini na madini ambavyo husaidia kuimarisha kinga ya mwili,
huongeza hamu ya kula chakula na kusaidia ukuaji vizuri, "anasema.
Anasema vitamini hivyo na madini vinasaidia kwenye uwezo wa kujifunza na kuimarisha afya kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa mifupa kupitia madini ya calcium.
"Tuna madini chuma ambayo yanasaidia katika utengenezaji wa damu na madini joto ambayo husaidia katika ukuaji mzuri wa kiakili, "anaeleza.
Anaongeza kuwa ili kijana awe na afya bora ni vizuri akala chakula kutoka katika makundi yote matano ya chakula bila kusahau maji ya kunywa.
Twin'omujuni anabainisha kuwa kundi la mwisho ni la mafuta, asali na sukari na kundi hilo linatakiwa kwa kiwango kidogo lakini lina umuhumu katika mwili.
"Lakini sambamba na makundi hayo matano tusisahau maji ya kunywa ambapo inashauriwa mtu kunywa kuanzi lita moja na nusu ila anaweza kunywa zaidi kulingana na shughuli anazozifanya, "anasema mtafiti huyo.
Anasema kazi za maji ni nyingi katika mwili ikiwamo kurekebisha joto la mwili, kusafirisha virutubishi ambavyo amevipata kwenye chakula.
Twin'omujuni anaeleza kuwa lishe bora kwa kijana balee inasaidia kuzuia uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama
vile magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu la juu.
Anasema kijana anatakiwa kula vyakula kutoka kwenye makundi hayo ya chakula kwa kiwango sahihi kulingana na kazi zake anazozifanya ili
kuweza kuuweka mwili katika hali inayostahili.
kuweza kuuweka mwili katika hali inayostahili.
Lishe duni
Twin'omujuni anasema lishe duni haistahili kwa kijana kwani inasababu nyinyi mojawapo ya sababu inayosababisha kijana kuwa na lishe duni
ni ulaji usiofaa mfano kula chakula kutoka kundi moja la chakula kwani kila kundi linakazi yake mwilini.
Anazitaja sababu nyingine zinazosababisha kijana kula chakula cha aina moja,kutokana na msukumo wa kundi rika kwa vijana hao kwani
katika kipindi hicho cha balee mwili hubadilika.
Mtafiti huyo anafafanua kuwa kipindi hicho cha balee kuna kuwa na msukumo wa kundi rika kwani anatakiwa kutengeneza umbo ambalo
linaweza kumsababishia kupata lishe duni na inaweza kuwa kiwango cha juu au chini cha lishe kitaalam zote ni lishe duni.
"Ngono zembe inaweza kumsababishia kijana kuwa na lishe duni anapokuwa katika kipindi hicho wanakuwa katika mihemuko kutokana na
mabadiliko yanayotokea mwilini ambapo hujaribu vitu toafauti tofauti, "anaongeza:
"Tunapokuja katika masuala la mahusianiano ndio kipindi ambacho anatamani kuwa na mahusuano na mtu mwingine ambapo anaweza kufanya
ngono zembe na kumsababishia kupata magonjwa yataokanayo na kujamiana
ikiwamo ukimwi, "anasema.
ngono zembe na kumsababishia kupata magonjwa yataokanayo na kujamiana
ikiwamo ukimwi, "anasema.
Matumizi ya vileo
Anasema lishe duni inaweza kutokana na matumizi ya vitu visiyostahili
mwilini mfano matumizi ya vileo, dawa za kulevya matumizi ya tumbaku pamoja na bidhaa zake kama vile ugoro.
Twin'omujuni anafafanua kuwa vitu hivyo vina athari kwa kijana na havistahili vinaweza ikamsababishia magonjwa ya mfumo kwa njia ya hewa ikiwamo kifua kikuu (TB ),Saratani na magonjwa mengine.
"Tunapokuja katika suala la kileo linapunguza hamu ya kula hivyo kijana balee hula chakula kidogo ambacho hakikidhi mahitaji yake pia
inaweza kumfanya awe mvivu asifanye kazi, "anabainisha.
Anaongeza kuwa kipindi cha kijana balee ni umri ambapo anatakiwa kujishughulisha na shughuli nyingi hivyo matumizi ya vileo yanaweza
kumsababishia kufanya ngono zembe kwani anakuwa hajatarajia.
Udandawazi
Anasema miaka ya leo kuna mabadiliko kwani dunia kwa sasa ni kama kijijini kijana anaingia kwenye mitandao ya kijamii akapakua vitu vya
ajabu ama akapendelea chakula kimoja alichokiona mtandaoni hali ambayo itamsababishia kukosa virutibishi na kumsababishia kupata matatizo kiafya.
ajabu ama akapendelea chakula kimoja alichokiona mtandaoni hali ambayo itamsababishia kukosa virutibishi na kumsababishia kupata matatizo kiafya.
Twin'omujuni anasema kuna madhara mengi yanayotokana na lishe duni
moja wapo ni upungufu wa damu ambao unatokea kwa vijana balee hasa wakike kwa sababu katika kipindi hicho wanaingia katika mzunguko wa
hedhi.
Anaeleza mzunguko huo husababisha kupoteza damu nyingi, kijana huyo anaweza kupata ujauzito wakati huo mahitaji yake ya mwili hayajitoshelezi ambapo anaweza kupata upungufu wa damu, kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu,kujifungua kabla ya wakati au mfu.
"Madhara menginie ya lishe duni ni kupata uzito uliozidi au kiribatumbo hali hiyo inaweza kumsababishia magonjwa sugu yasiyo ya
kuambukiza, "anaeleza.
Mbinu atakazotumia kuzuia
Anasema kuna mbinu ambazo anaweza kuzitumia kijana huyo ili kuzuia ikiwa ni ulaji unaofaa kula chakula kutoka katika makundi yote na kwa kiwango sahihi kulingana na shughuli za kijana huyo.
"Tunamshauri huyu kijana atumie mtindo bora wa maisha kwa kuepuka vile vitu ambavyo vinaweza kumsababishia kupata lishe duni, "anasema.
Anasema katika mtindo bora wa maisha kijana huyo anatakiwa kufanya mazoezi, kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuchangamsha mwili ikiwavni pamoja na kufua, kuosha vyombo na kulima bustani.
Twin'omujuni anaongeza kuwa mbinu nyingine ambayo anaweza kuitumia ni kula vyakula vya kundi la tatu ambalo ni mboga mboga na kundi hilo wengi hujua ni la watu wenye maisha duni kwa kua ni la mbogamboga.
Anasema kijana huyo pia anashauriwa kulisha shamba la mbogamboga iwe nyumbani au shuleni lakini pia atapata faida mara mbili kwa mbogamboga hizo na kufanya kuwa ni sehemu ya mazoezi na kupata chakula.
"Kumekuwa na dhana potofu wanapoulizana wenywe kwa wenyewe wanashidwa
kupata majibu sahihi ya ulaji wao hasa katika kipichi cha balee,"anasema.
Anasema kama kijana anaye penda kutumia chai anashauriwa kutumia vitu mbala vya asili kama mchai chai, tangawizi lengo ni kuepuka unywaji vyenye sukari nyingi na kahawa.
Twin'omujuni anaeleza kuwa vijana hao wanatakiwa kufuata maadili ya jamii kwa kujishughulisha mwili ikiwamo kufanya kazi.
"Tunawashauri vijana kuweka vyakula yao tangawizi ili kuweza kuwapatia hamu ya kula, " anasema.
0 Comments