WADAU WA MAZINGIRA WASHAURIWA KUTOA ELIMU MADHARA YA UKATAJI MITI


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MABADILIKO tabia nchi ni miongoni wa vitu vinavyoleta athari za ukame
nchini Tanzania na hata ulimwenguni kote,ikiwa ni Pamoja na ukataji miti hovyo.

Ni ukweli usiopingika Mataifa yaliyoendelea yanayochangia mabadiliko
ya hali ya hewa kutoka na shughuli za viwanda vikubwa vinavyochangia
kwa kiasi kuharibu Tabaka la juu la uso wa dunia yaani Ozone Layer.

wanasayansi wanakubali kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni ya kweli
asilimia 99, ya yamesababishwa na shughuli za kibinaadamu tangu mwaka
1850, wastani wa joto duniani umeongezeka kwa 1.1C.

Mabadiliko hayo ya tabia nchi yamesababisha madhara mbalimbali ikiwamo njaa kwa jamii ambayo ilizoea kuzalisha chakula kwa wingi na kunufaika hii inatokana na Shughuli za ufugaji ambazo kwa wafugaji kukosa
malisho ya mifugo yao ambapo hali hiyo imeharibu baadhi ya maeneo ya
kilimo.

kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia-WMO  joto limeendelea
kuongezeka duniani pamoja na kina cha bahari.

Mkoani Dodoma hali hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi  baadhi yao
wanaihusisha na suala la ushirikiana wanasema kuwa kuna ushirikina
ambao unazuia mvua huku wakitolea mfano  zamani  walikuwa wakilikuwa
ni heka moja  napata gunia  20 za mpunga, lakini kutokana na hali ya
sasa hivi, heka moja  wanaweza kupata gunia kumi, na wakati mwingine
wanakosa kabisa au wanapata kugunia 3.

Nuru Mohamed ni mkazi wa kijiji cha Daki kilichopo kata ya Mondo
wilani Chemba mkoani hapa ambaye ni mkulima wa zao la mtama na mahindi
na mfugaji anasema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri kwa kiasi
kikubwa shughuli z za kilimo.

Aefafanua kuwa alivyozoea kuvuna mazao mengi  na mifugo yake inata
sehemu ya malisho ambapo kwa sasa anakosa malishiio
“Mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa  yametuathiri sana sisi wakulima na
wafugaji. Zamani tulizoea mvua zikianza kunyesha  mwezi wa 10 na 11.

Wakulima tunakuwa tunalima lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
kwa sasa tunafika hadi mwezi wa kwanza mvua hakuna, aidha  inachelewa
kuja na kuwahi kuondoka hivyo kuacha mazao yakiwa  yamedumaa,” anasema
na kuongeza.

“Nashauri elimu itolewe ili tusilime kwa mazoea. Tuanze kulima kilimo
kinachoendana na  mvua ambayo inaendana na hali ya hewa kwa sababu
mpaka sasa tunaamini ya kuwa wananchi hatuna uelewa kuhusu masuala haya ya mabadiliko ya tabia nchi. Wengine wanafika mbali zaidi na
kuamini kuwa  mvua zinasababishwa na utawala wa kiongozi fulani kwa
wakati.

Hali hii imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha ukame katika baadhi ya maeneo ikiwemo Dodoma na hii
imesababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei ya vyakula ambavyo kwa sasa
vinauzwa kwa gharama ambayo wananchi wanashindwa kuimudu," amesema.

Naye Jamal Nyuki ni mkulima wa mazao mchanganyiko ikiwemo  karanga,
mtama na  mahindi kutoka kijiji hicho Dodoma, anasema kilio chake ni
kwa  serikali  pamoja na wadau wa mazingira nchini kuona ni kwa namna
gani wanaweza shirikiana katika kuhakikisha wanarudisha hali ya hewa
ya  mvua na mazao yashamiri kama ilivyokuwa zamani.

“Zamani tulikuwa hatutumii nguvu nyingi ukilima unajihesabia kabisa
wewe umepona na njaa, lakini siku  hizi tunaogopa hata kuwekeza nguvu
nyingi katika kilimo maana unaweka mazao mengi lakini wakati wa kuvuna
unaweza jikuta unavuna isifike hata kile kiasi cha mbegu ulichopanda
na zamani hata mbolea ilikuwa ni rahisi kuipata kwasababu mifugo
ilikuwa inapata malisho ya kutosha yanayozalisha mbolea.

“Wadau wa mazingira  tuwaombe watoe elimu kwa jamii ya namna ya utunzaji wa mazingira mfano huku kwetu suala la ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa  limeshamiri   kiasi kwamba mashambani siku hizi hakuna hata miti, wakati zamani  mashamba yalikuwa  yamejaa miti ya kivuli ukichoka kulima unapumzika,”anaesema Janeth.

Athari za mabadiliko ya tabia nchi zimejidhihirisha kwa zaidi ya miaka
50 sasa ambapo hali ya hewa duniani imekuwa ikibadilika, kwa sababu ya
kuongezeka gesi chafu zinazozalishwa na mvuke wa maji na hewa ya ukaa.
Gesi hizo zinatokana na kuungua kwa mafuta na makaa ya mawe, ukataji
wa miti na shughuli nyingine za kibinadamu kama kilimo na uchimbaji wa madini na shughuli za viwandani.

Bunge Tesa ni mwenyekiti wa kijiji cha Daki kilichopo jijini Dodoma amesema mchango wao katika kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira
ili  kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na kuzuia suala
la ukataji na uchomaji wa miti, na  mashamba ovyo bila utaratibu
maalum.

“Sisi tunaendelea kuhamasisha wananchi wapande  miti kwa wingi kwa
sababu zamani tulikuwa na mapori yenye  miti na ukisema unaenda porini
ni pori kweli.  Kwa hiyo tunahamasisha  upandaji miti katika kila nyumba na ninawachukulia hatua watu wanaochoma miti ovyo na
nimewaambia kabisa wananchi unapokata mti panda mti,” anasema Lungwa.

KAULI ZA MABALOZI WA MAZINGIRA NCHINI

Sakina Abdulmasoud ni balozi wa mazingira nchini Tanzania anasema kazi
yao mabalozi wa mazingira ni kuitafsiri kwa vitendo ajenda ya mazingira kwa kuhamasisha jamii ione umuhimu wake na kulifanya suala la upandaji wa miti kuwa ni utaratibu wao kawaida.

"Kama unavyofahamu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
inahamasisha upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kupitia
kampeni mbalimbali, ambapo sisi mabalozi jukumu letu kubwa ni kubeba
ajenda ile na kuisogeza kwa wananchi kwa ajili ya utekelezaji,"ameongeza.

“Kazi zetu tunazifanya moja kwa moja kwa jamii, kupitia utoaji wa
elimu mashuleni, uhamasishaji wa wananchi kwa kujumuika nao kwenye
shughuli za upandaji wa miti, lakini miongoni mwetu wapo waandishi wa
habari ambapo kupitia kalamu zao wanaelimisha jamii kwa kuwa
tunafahamu ili kuiokoa nchi yetu katika hatari ya mabadiliko ya tabia
nchi na kusababisha  ukame katika baadhi ya maeneo  mafuriko na
majanga mengine ni lazima tufanye kazi kwa ushirikiano,” ameeleza 
balozi Sakina.

Oliver Nyeriga nae pia ni  balozi wa mazingira anasema pamoja na
jitihada zao za kupambana kwa vitendo kuhamasiha suala la utunzaji wa
mazingira lakini  bado wana kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii kwani
kuna  baadhi yao ambao hawaoni haja ya utunzaji wa mazingira.

“Mfano sisi tunakwenda kwenye mitaa, masoko na  sehemu nyingine zenye
mikusanyiko ili kuhamasisha suala la utunzaji wa mazingira kwa kufanya
usafi lakini tunachotaka sisi jamii ione kama suala la utunzaji wa
mazingira si lazima wahamasishwe na mtu wafanye kama wajibu wao kama
yalivyo majukumu mengine wanayoyafanya ya kila siku bila kuhimizwa siku zote tunasema tunza mazingira yakutunze na usafi ni utu,” amesema Balozi Oliver.

WADAU WA MAZINGIRA

Njamasi Chiwanga  ni mkurugenzi wa miradi kutoka Shirika la LEAD
FOUNDATION lililopo wilayani Mpwapwa, Dodoma,  linalojishughulisha na
utunzaji wa mazingira  kwa  uoto wa asili  anasema wao wana  mchango
mkubwa  na kwa sasa wana mradi wa KISIKI HAI shuleni ambao  upo katika
shule 35 katika Mkoa wa Dodoma, Singida na Arusha unaosambaza  elimu
ya mazingira katika jamii.

“Sisi Lead Foundation  licha ya kuwa tunafanya suala hili katika
mazingira ya kawaida lakini pia tumeamua kuanzisha kampeni hii shuleni ili kuweza kuwafikia watoto, kuwabadilisha  fikra zao wakiwa wadogo
hata  wanapokuwa watakuwa mabalozi wazuri wa mazingira  na waswahili
siku zote husema samaki mkunje angali mbichi.

“Mradi huu tayari umeshatolewa muongozo  wake  shuleni  tunasema
lazima uanze kutunza mazingira ndipo uwaze kufikiria maendeleo ya kila
mtu mmoja mmoja.  Tunapokaa tukizungumzia   biashara unagusa
mazingira, afya, maji, elimu.

 Vyote  hivi vinagusa mazingira na sisi
kama Shirika tumemua kugusa agenda  za serikali katika utunzaji wa
mazingira,” amesema Chiwanga.

Chiwanga ameeleza  wao wanachofanya  hawapandi miti ila wanarudisha miti iliyokatwa kwa maana kisiki ambacho kipo hai ardhini lakini kilishakatwa juu wanakirudisha kinasimama tena na kuwa mti mkubwa
ambao unaishi.

WASIMAMIZI WA MISITU

Deosdedith Bwoyo ni  Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya
Maliasili na Utalii anasema  majukumu yao hasa ni kusimamia rasilimali
 za misitu, afya ya misitu, pamoja na kulinda hifadhi ya misitu
isiharibiwe.

Ameongeza kuwa  katika suala  la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wao kama wasimamizi  wakuu wa misitu katika ngazi zote,  wanapambana na
uharibifu ambao unafanywa na shughuli za  kibinadamu  ikiwemo kukata
miti au kufyeka  kwa ajili ya kupata mashamba, kuni, mkaa, mbao na
kadhalika.

“Mfano mtu anakuta kuna shamba la miti  ambalo limestawi na lina afya
sasa kutokana na haja yake yeye kwa wakati huo ya kutafuta mathalani
kuni au mbao anaingia anakata, na wengine wanafika mbali zaidi akikuta
kuna eneo ambalo limestawi vizuri kwa kuwa tu anaona kwamba akifyeka
pale kwa kuwa pamestawi anahisi akipatumia kwa kilimo patastawi na
kupata mazao mengi zaidi anaingia anakata na kuchoma.

Madhara haya ya  moto ambayo yamekuwa yakitokea katika baadhi ya
misitu hapa nchini yanafanywa na wananchi ambao wamekuwa wakikata miti kwaajili ya matumizi yao na niseme mimi kama Mkurugenzi wa misitu
licha ya kuendelea kuwachukulia hatua wale ambao wamekuwa wakifanya
uharibifu huo lakini elimu tunaendelea kuitoa juu ya utunzaji wa
misitu hii.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa utunzaji wa Mazingira Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Deosdetith Bwoyo amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa Wakala huo pia ni kuhakikisha uwepo wa usimamizi
madhubuti, wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki
unakuwepo na  kuongeza thamani ya mazao ya misitu na nyuki na kutoa
huduma bora kwa umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
utumishi wa umma.

Bwoyo amesema  dhima yao kuu ni usimamizi endelevu wa rasilimali za
taifa za misitu na nyuki ili kuchangia kikamilifu mahitaji ya kijamii,
kiuchumi, ki-ikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.

“Natoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu ovyo siku zote
tunapotunza hii misitu inakuja kututunza sisi mfano tukitembelea ndani
kwa kila mtu hapa nchini kwetu, unakuta ana meza ana kitanda ana
kabati hivi vyote vinatokana na miti hii ambayo ipo kwenye misitu sasa
ikikatwa zaidi itafika  tutakosa haya mahitaji,” anasema Bwoyo.
 

Post a Comment

0 Comments

KAMATI YA BUNGE SHERIA YAPONGEZA MAENDELEO YA MATUMIZI YA NeST