Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medali ikiwa ni wiki ya upandaji miti.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amesema matarajio ya serikali ni kupanda miti milioni 276 kwa mwaka na katika kila Halmashauri itatakiwa kupanda miti hiyo milioni 1.5 hivyo Watanzania wanatakiwa kutumia mvua zilizoanza kunyesha kupanda miti.
Pia Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuzindua Sera Mpya
ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 katika Maadhimisho ya upandaji miti.
Hayo ameyasema leo wakati wa zoezi la Upandaji wa Miti eneo la Medeli ikiwa ni wiki la upandaji miti amesema kuwa amefurahishwa na ile kauli "Soma na Mti ambapo wanafunzi wamejitokeza kupanda miti hiyo.
Waziri Jafo ameongeza kuwa serikali imeweka wiki maalumu ya upandaji miti kuanzia Febuari 7 na kwamba maadhimisho yake yafanyika Februari 12 mwaka huu na kwamba sera mpya ya mazingira ya mwaka 2021 itazinduliwa.
"zoezi la upandaji miti ndani ya Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimefarijika sana kuona wanafunzi kujitoa katika zoezi hili la kupanda miti," amesema Waziri Jafo
Ameeleza kwamba wanahakikisha muendelezo wa zoezi la upandaji miti linaendelea na kuwataka wananchi kutumia mvua kupanda miti ili kuhakikisha Kampeni ya Soma na Mti inafanya vizuri hapa nchini.
0 Comments