Monekano wa Saratani ya jicho Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WAZAZI wameshauriwa kuangalia macho ya watoto wao kwa lengo la kubaini dalili za kwanza za saratani ya mtoto jicho.
Saratani sio ungonjwa mzuri kwa sababu kupona kwake ni kama ikiwawahiwa kutibiwa.
Haya yalisemwa jijini Dodoma juzi na Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya, Dk.Bernadetha Shilio wakati wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari za afya kuhusu magonjwa yasiyoya kuambukiza alisema Saratani ya jicho la mtoto huwapata zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Alisema kiwango cha ukuaji wa Saratani hiyo ya jicho hukuwa zaidi kati ya umri huo na kuendelea hadi miaka mitano.
"Umri unapokuwa mkubwa hatari ya kupata ungonjwa wa macho inakuwa ni mdogo inaweza kuathirika jicho moja au yote mawili," aliongeza:
Kwa watoto mara nyingi wanacheleweshwa kufikishwa kwenye vituo vya afya na kwamba mzazi anapoulizwa anasema tangu alivyoonwa na mtaalamu hadi anafika katika kituo cha tiba ni miezi 11," alisema Dk. Shilio.
Alifafanua kuwa Saratani hiyo ukuaji wake ni wa haraka mno na kwamba ipo ndani sio rahisi kuonekana kwa kuwa mtoto anaonekana yupo vizuri na anaendelea anacheza kama kawaida.
Daktari huyo ameeleza kuwa dalili muhimu inayoonekana ni jicho kuwaka kwa ndani na ikiwa jioni linaonekana kuwa kama jicho la chui au paka.
Aliongeza kuwa mtoto anapoendelea kukua jicho linakuwa na kengeza na linaonekana kama lina mtoto wa jicho.
Dk.Shilio alisema kuwa jicho hilo linakuwa na weupe kwenye mboni na kati kati linaonekana kweupe.
Daktari huyo alibainisha kuwa Saratani inavyoendelea kukua inaathiri sehemu za kuta pembeni ya jicho, unapasuka na linavimba mtoto anaweza kutoka damu ndani ya jicho hilo.
" Baadae jicho linaathirika kabisa na linavyoendelea kuvimba linaathirika hadi kwenye maeneo mengine na mtoto anaweza kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa ripoti ya kwanza ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kuhusu Saratani ya jicho takribani watu milioni 2.2, Duniani kote Wana uoni hafifu au upofu kwa kukosa Huduma bora za afya.
Katika ripoti hiyo iliyozinduliwa nchini Geneva, Uswisi Oktoba 10, mwaka 2019, ilisema wagonjwa billion 1 kati yao wangeweza kupona kama wangepatiwa tiba mapema na huduma za afya au kinga.
0 Comments