ANATROPIA: HALMASHAURI YA KYERWA INA UPUNGUFU WA WATUMISHI ASILIMIA 75 KADA YA AFYA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MBUNGE  Viti maalumu Mkoa wa Kagera Anatropia Theonest ametaka kujua ni lini serikali  itapeleka watumishi wa kutosha katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa?

Anatropia ameuliza  swali la nyongeza  bungeni Aprili  27,jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ina watumishi kada ya afya 252 ikiwa na mahitaji ya watumishi 1022 ni pungufu ya asilimia 75.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius  Ndejembi amesema kuwa katika ajira ambazo  serikali imetangaza watahakikisha Halmashauri hiyo inapata watumishi  wa kada ya elimu na afya.

Aprili 12, mwaka huu jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki alitangaza ajira mpya katika kada za elimu na afya.

Idadi ya watumishi watakaoajiliwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi a Sekondari kada ya afya ni 8,070, ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vito vya Afya na Zahanati.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU