PROGRAMU YA ANAWEZA 'SHE CAN' IMEZINDULIWA DODOMA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima amemwakilisha
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kuzindua programu ya ANAWEZA 'SHE CAN' ambayo inalenga kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Programu hiyo imefadhiliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), na mpango huo utakagharimu fedha za Kimarekani Milioni 7.5,ambao unaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Akizungumza katika Mji wa kiserikali Mei 31,2023 wakati akizindua programu hiyo kwa  niaba ya Makamu wa Rais Dk Mpango amesema pamoja na kuwa wanawake ni tegemeo kubwa katika Taifa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mila na destruri zenye madhara, elimu duni na ukosefu wa mitaji na stadi za ujasiriamali. 

Dk. Gwajima ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia  imechukua hatua ya kuboresha kipato na kuondoa umaskini kwa wanawake na wanaume nchini. 


"Programu hii mekuja kwa wakati muafaka ambapo Tanzania ipo katika jitihada za kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi," amesema Dk. Gwajima.

Ameongeza kuwa kupitia Mfuko wa kuendeleza Wajasiriamali Nchini (NEDF), ulio chini ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), umewezesha mikopo kwa wanawake 1,026 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.35.

Dk.Gwajima amefafanua kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), unaosimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum umetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Milioni 664.5 kwa wanawake wajasiriamali 104 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili, 2023.
 
Ameeleza ni pamoja na kuwajengea uwezo wanawake ili bidhaa zao zikidhi vigezo vya ubora, ambapo Taasisi za SIDO, TBS na Wadau wengine wamewezesha wanawake kutengeza vifungashio bora na kuboresha biashara zao.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Kimataifa la Kifedha la Benki ya Dunia (IFC), amesema kuwa  hakuna uchumi unaoweza kufanikiwa bila mwanamke na kwamba programu hiyo imegharimu dola za kimarekeni milioni 10 amabo utatekelezwa katika mikoa mitano nchini.

"Leo tupo hapa kuzindua programu hii ya wanawake hapa Tanzania na Ina ongezeko la wanawake na nusu ya wanawake hawa ni wafanyabiashara ndogo ndogo," ameeleza Mkurugenzi huyo wa IFC.

Ameongeza kuwa  wanawake wanaofanya kazi za benki ni asilimia 12 tu na asilimia 34 ni wakulima.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii  Fatma Tawfiq amesema kuwa Bunge litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwawezesha wanawake kiuchumi.

"Mpango huu ni silaha ya ukombozi kwa mwanamke kujikwamua kiuchumi hivyo tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhakikisha Wanawake wanainuliwa kiuchumi," amesema.


Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa Rais wa Zanzibar Dk. Husein Ally Mwinyi anathamini kazi zinazofanywa na wanawake ambapo amekuwa akiwateu kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Ameeleza kuwa wanatambua jitihada zinazofanywa na serikali za kuhakikisha wanawake wanapata nafasi za uongozi na kwamba waliotangulia watawashika mkono wengi ili waende pamoja katika nyanja zote zikiwamo za kiuchumi.

Ameongeza kuwa ya muungano inathamini kazi zinazofanywa na wanawake ambazo zinalenga kuchochea Uchumi endelevu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI