SHIRIKA LA POSTA: MTEJA HATAKIWI KUFUATA MZIGO OFISINI ANAPELEKEWA ALIPO


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

SPIKA wa Bunge la Tanzania Dk.Tulia Ackson amesema kuwa Shirika la Posta Tanzania (TPC), linatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika kutoa huduma za vipeto,vifurushi na barua kwa kuwa limewezeshwa na anwani za makazi.

Hayo ameyasema Jijini Dodoma Mei 18,2023 katika viwanja vya Bunge kwenye maonesho ya watoa huduma za mtandao yalioandaliwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Tulia amesema kuwa amefurahishwa na zoezi la anwani za makazi ambalo lilianzia mapema mwaka jana na kwa sasa wamefikia sehemu ambayo kwa yule aliyesajiliwa namba yake anaweza kuipata kiganjani kwa kutumia aina yoyote ya simu.

"Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na Wizara hii ya habari mtu kujua anwani yake ya makazi ni jambo la msingi sana.,"ameeleza.

Aidha amewataka wananchi ambao bado hawajasajili makazi yao ni muhimu kupata anwani za makazi ambazo zinasaidia katika maendeleo ikiwa ni pamoja na kuliwezesha Shirika la posta katika utendaji kazi wake.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Posta Kimataifa, Elia Madulesi amesema kuwa wanazo anwani za makazi ambazo mfumo wake upo tayari na kwamba wao kama Shirika hilo wamefanya kila mtanzania aweze kujulikana alipo.

Ameongeza kuwa katika kutoa huduma za vipeto,vifurushi na barua wanamfikia mwananchi, mteja hadi nyumbani kwake kwa kujua anwani yake na alipo hivyo mwananchi huyo hahitaji tena kwenda Posta kuwatafuta bali wao ndio watamtafuta.

Meneja huyo amesema anwani za makazi zinawawezesha kuwafikia wateja wao walipo na kwamba wanampunzia mteja muda wa kuwafuata.

"Tupo hapa kwenye viwanja vya Bunge tukiwa na maonesho haya tukiwaelezea wananchi na waheshimiwa wabunge namna Shirika la posta limejinasibu hasa katika kwenda kidigitali, nianze kwa kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameweka msisitizo kwa ajili ya kuwafikia wananchi kwa huduma mbalimbali," amesema

Amefafanua kuwa maendeleo yanakwenda haraka kutokana na serikali kuwekeza na wao inawawezesha kutoa huduma kwa urahisi kwa wananchi, wateja.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI