Na mwandishi wetu, Dar es salaam
SEKTA ya ujenzi hapa nchini imezidi kukua siku baada ya siku ambapo watanzania wataweza kukutana na makampuni mbalimbali bora ya vifaa vya ujenzi kutoka hapa nchini na yale ya nje ya Tanzania.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam leo Oktoba 11,2023 na Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfray Kasekenya wakati akifungua Maonesho ya Dar Construction Expo 2023, amesema
maonesho hayo ni muhimu kwa kuwa yanawakutanusha wadau mbalimbali wa ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi.
Aidha katika hatua nyingine ameipongeza bodi ya wakandarasi hapa nchini kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali yakiwemo madaraja na barabara zenye ubora hali iliyopelekea Taifa kuwa na Miundombinu bora.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo,muandaaji wa maonesho hayo Deogratius Kilawe amesema Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia leo Tarehe 11- 13 Oktoba 2023 ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.
Amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu katika kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi.
0 Comments