MKUTANO WA AGRF ULIVYOWANUFAISHA WADAU WA SEKTA YA UFUGAJI NA UVUVI

Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WADAU wa sekta za mifugo na uvuvi wamekiri kunufaika na mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF),ambapo asilimia 61 wameonesha kupata masoko mapya ya bidhaa wanazozalisha, asilimia 54 wamepata uwekezaji mpya, asilimia 82 wameweza kutangaza Kampuni au bidhaa zao kwa wadau mbalimbali waliokutana nao.

Mkutano huo ambao umefanyika Septemba 5 hadi 8, 2023 jijini Dar es salaam na kuongonzwa na Rais 
Dk.Samia Suluhu Hassan huku 
anga la Tanzania likijaa mazungumzo kuhusu mustakabali wa mfumo wa chakula barani Afrika kwenye mkutano huo.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 02,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkutano huo wa AGRF, amesema 
Katika kikao kilichofanyika  Septemba 29 mwaka huu kwa njia ya mtandao ambapo  Wizara ilikutana na wadau 311, kutoka katika hiyo.

Ameeleza kuwa asilimia 100 ya wadau wote walioshiriki katika maonesho ya bidhaa, wamekiri kupata mauzo mengi ya bidhaa zao katika kipindi cha mkutano wa AGRF na kwamba asilimia 98 ya wadau wameonesha kunufaika na mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa mkutano huo  ikiwemo elimu ya namna ya kuongeza tija katika biashara, teknolojia za uzalishaji na uchakataji, fursa za kupata rasilimali fedha na namna ya kuyafikia masoko.

Waziri huyo ameeleza kuwa uwepo wa wadau 5,400 kutoka nchi 90, ulionyesha ushirikiano wa kimataifa ulioimarika wa Tanzania.

Ameongeza kuwa uwekezaji katika sekta ya mifugo na uvuvi, kwa kuzingatia mazingira endelevu, ni kipaumbele chao.


"Tunaamini kwamba kwa kushirikiana na wenzetu, tunaweza kufikia lengo letu la kuwa na mfumo wa chakula ambao ni endelevu, wenye usawa, na unaowezesha maendeleo ya kiuchumi kwa wote," ameeleza Waziri huyo.

Ameongeza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa sekta ya mifugo na uvuvi zinachangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa Tanzania na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Waziri Ulega amefafanua kuwa AGRF 2023 iliangazia vijana na wanawake kama msingi wa chakula cha baadae Afrika huku akisema Biashara za ndani ya  nchi zimejenga daraja na wenzao wa kimataifa, zikichora njia za uwekezaji na ushirikiano.

Akizungumzia upatikanaji wa Rasilimali Fedha za Ufadhili wa Programu ya Building Better Tomorrow ( BBT), amesema Tanzania ilipata fursa ya kuonesha program bunifu ya BBT,(Presidential Legacy Project ) Kiasi cha Dola za Marekani milioni 500 zilitolewa kama ahadi kwa ajili ya kufadhili programu hiyo kwa sekta za uzalishaji.

"Napenda kuwahakikishia wawekezaji wa kimataifa kwamba Tanzania ina fursa nyingi katika sekta ya mifugo na uvuvi ambazo bado hazijaguswa. Serikali yetu imejitolea kutoa mazingira rafiki kwa wawekezaji, na tuko tayari kushirikiana nanyi katika kila hatua," ameongeza.

Nchi yetu ina rasilimali, ardhi, na mazingira yanayofaa kwa shughuli za mifugo na uvuvi, na sasa tunaweka mkazo kwa teknolojia na mafunzo ili kufikia viwango vya kimataifa,": amesema.

Aidha ametoa shukrani zaje za dhati kwa wote walioshiriki katika jukwaa hilo ikiwa ni pamoja na wadau wa kimataifa, wawekezaji, vijana, wanawake na wenzangu wote serikalini.

"Napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake thabiti na imani yake isiyo na kifani kwa mustakabali wa Tanzania," amesema.

Waziri Ulega amebainisha kuwa Sekta ya mifugo inachangia takribani asilimia 7.4 ya Pato la Taifa la Tanzania hata hivyo hilo halionyeshi picha kamili ya kiuchumi, ambayo inajumuisha thamani ya bidhaa za mifugo zinazotumiwa ndani ya nchi na mapato kutoka kwa mauzo ya nje ya mifugo, kwa hivyo jitihada zaidi na utafiti unahitajika na bilashaka hii itakuwa imeongezeka. 

Amesema zaidi ya watu milioni 10 Tanzania wanajihusisha na ufugaji na uvuvi, ikiwa ni pamoja na wafugaji, wakulima wadogo, na wafugaji wa kibiashara.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI