WAYIMPEX WAJIVUNIA USAFIRISHAJI WA ZAO LA KOROSHO NJE YA NCHI


Na Andrew Chale, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya usafirishaji wa mizigo nje ya Nchi na upokeaji mizigo ndani ya nchi ya Wayimpex inayojihusisha na masuala ya Forodha yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam, imejivunia ubora wa usafirishaji bidhaa za mazao ya kilimo ikiwemo Korosho, Ufuta, Mbahazi, kunde na mengineo kutoka Tanzania kwenda nchi za India na Malaysia katika kuinua uchumi Nchini

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano wa Kimataifa wa zao la Korosho unaofanyika katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Afisa biashara wa kampuni hiyo ya Wayimpex, Dickson Mshana amesema tokea wameingia katika soko la ushindani wameweza kufanya vyema na wanawashukuru wadau na wateja kwa kufurahia huduma zao ya kusafirishiwa mazao nje ya nchi.

‘’Hapa nchini tuna ofisi mbili, moja Jijini Dar es salaam na nyingine pale bandari ya Mtwara ambapo tuna ofisi yetu na tunashughulikia kwa kiwango kikubwa zaidi suala la usafirishaji ikiwemo zao hili la korosho na mbahazi.

Wayimpex imejidhatiti kuhakikisha mazao yote ya biashara yanasafirishwa kwa ubora wa kisasa ilikulinda soko letu’’ amesema Mshana.

Ameongeza kuwa, mazao ya kibiashara kama Korosho wanasafirisha nje ya nchi hali inayoendelea kukuza tija la zao hilo la Kitaifa linalolimwa kwa wingi Mikoa ya kusini. 

Aidha, amebainisha kuwa, Wayimpex ni miongoni mwa makampuni bora nchini ambapo lengo lao kuhakikisha wanaisaidia jamii katika kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi, kwa njia bora na ya kisasa ikiwemo njia ya uhifadhi na upakiaji mpaka kumfikia mteja nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU