Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Mb), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.Doto Biteko pamoja na mawaziri na wabunge mbalimbali wakimpongeza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Wizara,Mhandisi Maryprisca Mahundi baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2024/2025 bungeni jijini Dodoma leo Mei 16, 2024.
Na Asha Mwakyonde
SERIKALI Kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi zaidi Bilioni 100,700,000,000 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato vya wizara ikiwepo mauzo ya huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Akiwasilisha hotuba yake ya Mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 leo Mei 16,2024 bungeni Jijini hapa Waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye amevitaja vyanzo vingine vya mapato kuwa ni makusanyo yatatokana na ada ya usajili wa Magazeti, ada ya mwaka ya magazeti, vitambulisho vya waandishi wa habari na machapisho ya picha, mabango na majarida.
Amesema, mbali na makusanyo hayo, Wizara imeandaa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2024/25 kwa kuzingatia, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Waziri huyo amefafanua kuwa bajeti hiyo imezingatia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22-2025 2026, na hotuba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia Bunge, Aprili 22, 2021.
0 Comments