Na Asha Mwakyonde, DODOMA
KATIKA ulimwengu wa sasa ambapo mwonekano na kujiamini vina mchango mkubwa katika maisha ya kila siku, huduma za urembo zimekuwa hitaji muhimu kwa watu wa rika zote.
Mari House of Beauty imejipambanua kama kituo bora kinachotoa huduma za kisasa za saluni kwa ubora wa hali ya juu, zikilenga kumfanya mteja ajisikie thamani na kuonekana nadhifu kila wakati.
Saluni hii inatoa huduma mbalimbali zinazokidhi mahitaji tofauti ya wateja, kuanzia urembo wa nywele hadi utunzaji wa ngozi. Huduma hizo ni pamoja na facial treatment, kuchora nyusi kwa uzi, waxing, kope, huduma zote za nywele pamoja na kupamba maharusi.
Mmiliki wa Mari House of Beauty, Mariam Sweya anasema ndani ya saluni ya Mari House of Beauty, vipodozi mbalimbali vinapatikana. Kwa upande wa nywele, wateja hupatiwa huduma za kusuka mitindo ya kisasa, kufunga nywele (weave na wigs), kupaka rangi, kukata na kutengeneza nywele kwa ustadi mkubwa.
Anafafanua kuwa Wataalamu waliopo wana ujuzi wa hali ya juu na hufuata mitindo ya kisasa, lengo likiwa ni kuhakikisha kila mteja anapata huduma inayomridhisha.
Mbali na huduma za nywele, anaeleza kuwa Mari House of Beauty pia hutoa huduma za urembo wa uso na ngozi, ikiwemo usafishaji wa ngozi (facial) na make-up kwa ajili ya hafla mbalimbali kama harusi, sherehe na vikao rasmi.Anasema huduma hizo husaidia kuboresha afya ya ngozi pamoja na kuongeza mvuto wa muonekano wa mteja.
Aidha, anaongeza kwamba huduma za manicure na pedicure hutolewa kwa umakini mkubwa, zikilenga kuhakikisha kucha za mikono na miguu zinakuwa safi, zenye afya na muonekano wa kuvutia.
"Vifaa vinavyotumika ni safi na vya kisasa, jambo linalohakikisha usalama wa wateja wakati wote," anasema Sweya.
Sweya anaeleza kuwa kinachoitofautisha Mari House of Beauty na saluni nyingine ni huduma bora kwa wateja, mazingira safi na rafiki, pamoja na matumizi ya bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Anasema Wateja hupokelewa kwa heshima na kuhudumiwa kwa weledi, hali inayowafanya wengi kurudi tena na tena.
Mari House of Beauty si saluni tu, bali ni sehemu ya kupata huduma za urembo na kituo cha kujenga kujiamini na kuboresha mwonekano wa kila mteja. Ni chaguo sahihi kwa yeyote anayetafuta huduma bora, za kisasa na zenye thamani halisi ya fedha.



0 Comments