KIHONGOSI AVALIA NJUGA MIKOPO KAUSHADAMU


Na Mwandishi wetu 

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaowadhulumu wanawake kupitia mikopo yenye riba kubwa maarufu kama mikopo kaushadamu. Kihongosi ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji wa Katoro, mkoani Geita. KiongozI huyo amesikitishwa na taarifa za kuwepo kwa mikopo yenye masharti magumu yanayoumiza wananchi. 

" Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia ujanja wa kutoa mikopo yenye masharti kandamizi, hali inayowafanya wakopaji hasa wanawake kupoteza fedha na mali zao kutokana na riba kubwa na masharti yasiyo rafiki." “Nimesikitishwa kusikia hapa Katoro kuna mikopo kaushadamu, nakuagiza DC wanaodhulumu wanawake washughulikiwe kwa sababu tukiruhusu hali hii iendelee, wananchi wengi watapoteza fedha na mali zao." 

Pia amemuelekeza DC Komba kuhakikisha anasimamia na kudhibiti vitendo hivyo kwa ukaribu na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.

Kihongosi amewahimiza wananchi hususan wanawake kuwa waangalifu na kuepuka kujiingiza katika mikopo yenye masharti magumu ambayo inaweza kuwaingiza katika hasara na kuathiri ustawi wao wa maisha. 

Pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendesha shughuli halali za kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

0 Comments

SIASA NI HESABU, MTAJI WA WANACHAMA WAIBEBA CCM