KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amesema siasa ni hesabu na kuwa nguvu ya ushindi kwa chama hicho inatokana na idadi kubwa ya wanachama waliopo ngazi ya shina.
Kihongosi ameyasema hayo alipotembelea na kuzungumza na wananchi pamoja na wana-CCM wa shina namba 12 lililopo Geita Vijijini mkoani Geita.
Akitolea mfano shina hilo, amesema lina wanachama hai takribani 200 na kwamba Wilaya ya Geita Vijijini ina mashina 3,614, hali ambayo ni nguvu kubwa inayoipa CCM ushindi wa wazi wakati wa uchaguzi.
“Hivyo, siasa ni hesabu. Ukiangalia hapa tu kuna wanachama kama 200, ukizidisha kwa mashina yote unapata idadi kubwa sana. Mwambie kuwa sisi tunashinda kwa sababu tuna watu.”
Amesema wananchi, wakiwemo wa Bugulula, wanachohitaji ni maendeleo kama barabara, umeme, shule, hospitali na huduma za kilimo badala ya vurugu za kisiasa.

0 Comments