Mfumuko wa bei wapungua kwa bidhaa zisizo za vya kula



Kaimu Mkurungenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja akizungumza na waandishi wa habari

Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Januari na kwamba 2022 umepungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka 4.2 kwa mwaka ulioishia Disemba 2021.
Haya yameelezwa jijini Dodoma leo Febuari 8, mwaka huu na Kaimu Mkurungenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja amesema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari.
Amesema kuwa mwaka 2022 mfumuko huo umepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo  kwa mwaka ulioishia Disemba 2021.
" Kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, mwaka 2022 kumechangiwa hasa na mfumuko wa bei  wa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Januari, mwaka 2022 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021," amesema Minja.
Ameongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula  na vinjwaji baridi  kwa mwaka 2021, mwaka 2022 umepungua hadi kufikia asilimia 3.1 kutoka asilimia 3.9 ilivyokuwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021.
Minja amefafanua kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula visivuochakatwa Nishati na bili za maji (Core inflation), kwa mwezi Januari mwaka 2022 umepungua hadi aslimia 4.4 kutoka 4.6 ilivyokuwa mwezi Disemba 2021.
Ameeleza kwamba baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula  zilionesha kupungua kwa mfumuko wa bei mwaka ulioishia mwezi Januari, mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 ni pamoja na mavazi kutoka asilimia 4.5 hadi kufikia 2.8.
Ameongeza kuwa bidhaa ninyine ni viatu kutoka aslimia4.6 hadi kufikia asilimia 4., Kodi ya pango kutoka asilimia 4.4 hadi 1.2, magodoro kutoka asilimia 12.3 hadi 7.3, majokofu kutoka asilimia 4.2 hadi 1.5, cherehani kutoka asilimia 9.1 hadi 5.0, simu janja kutoka asilimia 4.6 hadi 3.3, vyombo vya nyumabani kama sahani kutoka asilimia 16.7 hadi 3.6.
"Bidhaa nyingine zilizopungua bei ni Runinga kutoka asilimia 3.5 hadi 1.2 na malazi kwenye hoteli  na Nyumba za kulala wageni  kutoka asilimia 6.6 hadi 2.9," amesema.

Post a Comment

0 Comments

KAMATI YA BUNGE SHERIA YAPONGEZA MAENDELEO YA MATUMIZI YA NeST