Waziri Simbachawene: wananchi tumieni Tume ya haki za Binadamu kutatua matatizo ya kisheria






Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari

Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawene amesena kazi ya Tume Haki za Binadamu na Utawala Bora ni kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ili wapate haki zao msingi za kisheria.
Pia amewataka wote 
wanaohisi ndugu zao wamekosa haki na kuonewa,waliopo mahabusu na Magereza kwenda katika Tume hiyo Ili kupata
msaada wa kisheria.
Akizungumza jana wakati wa ziara ya katika Tume hiyo Simbachawene amesema asingependa kuona watu wanaishia kulalamika
mitaani ilihali Tume hiyo ipo na kazi yake ya kutoa msaada wa kisheria
kwa taasisi,mtu mmoja moja na umma.
"Kuanzia leo wananchi
mjipange kuja katika Tume hii kupata msaada wa kisheria ambao
utawasaidia kujua nini wafanye ili wapate haki zao,"ameongeza.
“Nawaomba muitumie Tume kuhakikisha mnasaidiwa masuala ya kisheria ili muweze kuendelea na shughuli zenu," amesema Simbachawene.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa serikali kuwaelekeza watu wenye
changamoto mbalimbali kuwaelekeza jamii umuhimu wa chombo hiko ndani
ya wananchi.

"Haki za binadamu ni ajenda ya kimataifa, tunawakaribisha Watanzania pale wanapokuwa na changamoto  zozote zile taasisi hii itawasaidia kwa kuwasikiliza,”ameongeza.

Amesema  hiyo imeundwa kwa mujibu wa katiba na sheria wananchi wana ndugu zao ambao wapo katika mahabusu na magereza inapotokea hatua ya wao kushindwa chombo hicho kina wajibu wa kutembelea kujua hali ya maisha ya binadamu ambao wanaishi katika maeneo yaliyo zuiliwa.

Waziri huyo ameeleza kuwa kuanzia sasa anahitaji kuoa chombo kinakuwa maarufu kwa kujitangaza,huku akiwataka vyombo vya habari kusaidia kutoa taarifa ili wananchi waitumie Tume hiyo kutatua changamoto mbalimbali.
Akizungumzia kuhusiana na Ripoti za Tume hiyo kufikishwa Bungeni
Simbachawene ameahidi kuanzia sasa ripoti hizo zitafika na kusomwa Bungeni kama zilivyo ripoti za taasisi nyingine.
“Niwahakikishie mimi kama Waziri mwenye dhamana,kama Ripoti mnazo leo basi kesho zitazifikisha Bungeni ili zisomwe,”alisema Simbachawene.
Waziri Simbachawene amesema Tume hiyo inapaswa kujulikana na kuwa maarufu kwa sababu
inafanya kazi za kutafuta haki za Binadamu ambao wanahitaji saada wa kisheria ili kupata haki zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema Tume hiyo imefurahishwa na serikali
kuwaongezea bajeti shilingi bilioni 1na kufika bilion 3.
"Pamoja na kuongezewa bajeti fedha hizi lakini bado
hazitoshi tunahitaji kuwa na bajeti ya bilioni 6 ili tuweze
kukidhi mahitaji na kufikia maeneo ambayo hatujayafikia kwa ajili ya
kutatua changamoto za wananchi," amesema.
Aidha Jaji Mwaimu amesema wanaiomba Serikali kuongeza wafanyakazi ili kuongeza nguvu ya kiutendaji katika kazi zao za kila siku ambazo wanatakiwa kufanya.
Amesema Tume hiyo imekuwa na Ushirikiano mzuri na wadau wa maendeleo kwa kiasi kikubwa imewaongezea ufanisi katika utekelezaji wa miradi ambayo inasimamiwa na Tume.

Post a Comment

0 Comments

KAMATI YA BUNGE SHERIA YAPONGEZA MAENDELEO YA MATUMIZI YA NeST