RAIS SAMIA APONGEZWA MIRADI YA MAENDELEO KILIMANJARO

Na Mwandishi wetu -Kilimanjaro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi kubwa anazozionesha za kuruhusu kuendelea ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kwa kutoa shilingi Bilioni 51 kutekeleza miradi katika Wilaya ya Mwanga.

Pongezi hizo zilitolewa na Mbunge wa Viti Maalum kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akiendelea na ziara yake katika Tarafa ya Mwanga, Lembeni na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Jipe-Ndea, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri huyo alieleza kwamba Mhe. Dkt. Samia ameendelea kujali wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu kwa kujenga mabweni 80 Nchi nzima kwa huku akimpongeza kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mwanga na mradi mkubwa wa maji katika Wilaya mbalimbali za Mkoa huo.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametujali sana watu wa Kilimanjaro na hapa Mwanga , kuna wakati alisema sherehe za uhuru zisifanyike na kuelekeza fedha hizo kutumika kujenga mabweni 80 Nchi nzima kwa lengo la kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye ulemavu,”Alipongeza Mhe. Nderiananga.

Vile vile aliwahimiza wazazi na walezi wenye Watoto wenye ulemavu kuendelea kuwathamini na kuwapeleka shule ili waweze kusoma na kutimiza ndoto zao akisema wakipewa nafasi wana uwezo wa kufanya mambo makubwa katika jamii.

Mhe. Nderiananga aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpigakura na Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi na wao kuchaguliwa huku akisihi wanawake kujitokeza kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji ili nao washiriki katika nafasi za naamuzi. 

Katika hatua nyingine alizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki kufuatia uwepo wa changamoto ya Wanyama hasa tembo ambao wamekuwa wakiwajeruhi wananchi wa Kata ya Kwakoa na kuharibu mazao yao ambapo Mhe. Kairuki aliwataka kuwa makini kwa kufuata utaratibu ambao wamekuwa wakipewa wakati serikali ikifanyia kazi changamoto hiyo. 

Kwa upande wake Afisa Tarafa-Mwanga Bi. Zawadi Mirambo alieleza kwamba wananchi wanabudi kujivunia kutokana na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao akisema Wilaya imepokea shilingi Bilioni tatu kujenga hospitali ya Wilaya ya Mwanga, ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA).

“Hospitali imeanza huduma ya (OPD) na tunaendelea kupokea vifaa ili kutoa huduma zote za kiafaya, kam ahaistoshi tuna mradi wa Veta ambapo tuimepokea Bilioni 3 ili Watoto wetu weweze kusoma fani mbalimbali na tunamshukuru pia kwa mradi wa maji Wilaya ya Same, Mwanga na Korogwe pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Toroha,” Alifafanua Afisa Tarafa huyo.

Naye Diwani wa Kata ya Kwakoa Bwa. Kiende Mvungi alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi Milioni 43 mwaka 2023 ili kujenga madarasa ya kupokea wanafunzi kidato cha kwanza, shilingi Milioni 77 kwa jili ya ujenzi wa madarasa shikizi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU