Na Mwandishi wetu,DODOMA
KATIKA kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za Msaada wa Kisheria kwa wakati na Usawa, Wizara ya Katiba na Sheria imeanza kutekeleza rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili Mkoani Dodoma kwa lengo la kutoa huduma za kisheria na elimu kwa wanachi wote hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za huduma za Kisheria.
Katika awamu ya pili ya utekelezaji Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi mbalimbali katika mnyororo wa haki jinai zinazoshiriki kutekeleza Kampeni hii zitatoa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri wa kisheria, utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo Migogoro ya Ardhi, Ndola,Mirathi, matunzo ya watoto na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria katika mkoa wa Dodoma inatekelezwa kwa muda wa siku kumi na tano katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma zikiwemo Kata,Mitaa na Vijiji vyote vilivyopo katika Halmashauri hiyo bila malipo.



0 Comments